RATIBA YA KICHUNGAJI YA BABA ASKOFU 2016

KALENDA YA SHUGHULI ZA KICHUNGAJI ZA BABA ASKOFU

NA MATUKIO MAALUM:  JAN – DES 2016

Mwaka wa Nane wa Jimbo Katoliki la Kayanga:  2016

 

MPANGO MKAKATI: KUOMBA HURUMA YA MUNGU NA KUIMARISHA MAISHA YA SAKRAMENTI NA MATENDO 14 YA HURUMA.

 

JANUARI 2016: KUUNDA UPYA  JNNK NA UHAMASISHAJI WA SAKRAMENTI YA NDOA NA KUBARIKI

NDOA KWA VIONGOZI TARAJIWA WA JNNK.

1 Ijm:  SHEREHE ZA MWAKA MPYA 2016: “YANGUHA”.

17 Jmp: Kusimikwa Askofu Titus Mdoe kuwa Askofu wa Mtwara.

19 Jmn: Ufunguzi wa Mwaka wa Shule: Misa St. Peter Claver EMBP/School.

23 Jms: Ufunguzi wa Mwaka wa Shule: Misa St. Augustine Kaisho Sec. School.

25 Jmt: DARAJA LA USHEMASI: Frt. Jacobus Mwita na Frt. Julius Mugisha, Parokiani

Ndorage.

31 Jmp: HIJA NJE YA JIMBO, KISHOMBERWA, MINZIRO.

        – Muhimu: Wasilisha Jimboni @ mwisho wa mwezi 20%:10% Sadaka, 5% Zaka  na

5% Utume wa Walei.

– Tangazo la kuleta Matawi yaliyobarikiwa mwaka jana kwa ajili ya Jumata    no ya Majivu

 

FEBRUARI 2016: UCHAGUZI HAWAKA: NGAZI JNNK.

2 Jmn: Kutolewa Bwana Hekaluni: KUHITIMISHA MWAKA WA WATAWA. Kanisa Kuu.

2 Jmn – 10 Jmo: Novena ya Bikira Maria wa Lurdi kwa ajili ya Hija Lurdi-Bugene

(11 Februari).

5 Ijm: Ijumaa ya Kwanza ya Mwezi – Moyo Mtakatifu wa Yesu “Benediction after      Holy Mass”.

6 Jms:  Mkutano wa Bodi CHUDIKYE kufanyika Kayanga – CHEMA.

9 Jmn: Uzinduzi wa miaka 60 (26/02/1956)  Parokia ya Rwambaizi.

10 Jmo: JUMATANO YA MAJIVU: Siku ya kufunga na kutokula nyama.

Mfungo wote wa KWARESIMA – Sherehe, burudani, ngoma, muziki, starehe na pombe haviruhusiwi. Ni wakati wa kujitakatifuza, kujinyima kwa ajili ya kusaidia maskini, yatima, Kanisa kwa kulipa zaka 10% ya Kanisa, sadaka na michango mbalimbali; kusali na kupokea Sakramenti na kujilisha Neno la Mungu.  Kila Ijumaa Njia ya Msalaba na michango ya kusaidia Nchi Takatifu na wahitaji.

11 Alh: HIJA YA 5 LURDI-BUGENE: Bikira Maria wa Lurdi: Yubilei ya  Wagonjwa na wasiojiweza (Zitatolewa Sakramenti za Kitubio na Mpako wa wagonjwa).

12 Ijm: Ibada ya Njia ya Msalaba – jioni.  Picha za Njia ya Msalaba zisimikwe vizuri

katika Makanisa yote.

14 Jmp – 20 Jms: MAFUNGO YA MWAKA YA MAPADRE.

 

MACHI 2016:  UCHAGUZI HAWAKA: NGAZI JNNK.

1 Jmn – 2 Jmo: Bishops’ Metropolitan Meeting – Mwanza.

4 Ijm: Workshop on the Protection/care of minors/priests of Bukoba, Kayanga,

Rulenge-Ngara to meet in Bukoba.

– Ijumaa ya Kwanza ya Mwezi – Moyo Mtakatifu wa Yesu “Benediction after Holy Mass”.

– Ibada ya Njia ya Msalaba jioni.

5 Jms: “Masaa 24 kwa ajili ya Bwana”  (Kuanzia Ijumaa).

11 Ijm: Ibada ya Njia ya Msalaba jioni.

14 Jmt: Pro-Life Tanzania:  Mafunzo ya Utetezi wa Uhai kufanyika CHEMA. Kila

parokia itume wajumbe 5 wakiongozwa na mapadre wao.

18 Ijm: Ibada ya Njia ya Msalaba jioni.

19 Jms: Sherehe ya Mt. Yosefu, Mume wa Bikira Maria.

20 Jmp: JUMAPILI YA MATAWI: Sikukuu ya Vijana Ulimwenguni: Michango na

Minada kuimarisha Umoja wa Vijana Vigangoni, Parokiani na Taifani. Kumbuka:              “Zizi bila ndama hutoweka”.

22 Jmn:  MISA YA KRISMA:  Kanisa Kuu Kayanga: Hamasisha Watawa, Makatekista na

Waamini wote kuhudhuria.

24 Alh: ALHAMISI KUU: Misa jioni saa 10.30 na kuabudu hadi saa 6.00 usiku.

–  Shukrani kwa kuwekwa Sakramenti ya Ekaristi na Upadre.  Kuwaombea  Mapadre.

25 Ijm: IJUMAA KUU: Ibada saa 9.00: Siku ya kufunga, kutokula nyama na kujitolea

Parokiani/Kigangoni.  Michango ya kusaidia Nchi Takatifu. Kuanza Novena ya Huruma  ya Mungu.

26 Jms: JUMAMOSI KUU: MISA YA VIJILIA YA PASAKA: Ubatizo wa Wakatekumeni

waliosajiliwa Kwaresima 2015.

27 Jmp: JUMAPILI YA PASAKA

28 Jmt: JUMATATU YA PASAKA

 

APRILI 2016:  UCHAGUZI HAWAKA VIGANGO.

1 Ijm: Ijumaa ya Kwanza ya Mwezi – Moyo Mtakatifu wa Yesu “Benediction after Holy Mass”.

3 Jmp: JUMAPILI YA HURUMA YA MUNGU.

7 Alh: Karume Day.

17 Jmp: MIITO MITAKATIFU: Kuombea, kuhamasisha na kufadhili Miito katika Kanisa         .                              – Parokia kubadilishana Wahubiri. C/o Vocations Director.

23 Jms:  Sherehe ya Mt. George Msimamizi wa Parokia ya Kanisa Kuu, Kayanga.

26 Jmn: Sikukuu ya Muungano.

 

MEI 2016: UCHAGUZI HAWAKA UNAENDELEA NGAZI YA VIGANGO.

1 Jmp: Sikukuu ya Wafanyakazi: Jubilei ya watenda matendo ya Huruma: Kubariki vyombo

vya kazi na mikono.

6 Ijm: Ijumaa ya Kwanza ya Mwezi – Moyo Mtakatifu wa Yesu “Benediction after Holy Mass”.

– Novena ya Roho Mtakatifu (PENTEKOSTE).

14 Jms: MT. MATHIAS:  Sikukuu ya UMAWATA.

15 Jmp: PENTEKOSTE: Michango ya kuimarisha HALMASHAURI YA WALEI (HAWAKA).

22 Jmp: UTATU MTAKATIFU.

29 Jmp: EKARISTI TAKATIFU.

 

JUNI 2016:  UCHAGUZI HAWAKA  PAROKIA.

1 Jmo – 5 Jmp:  Kongamano la Kitaifa la Ekaristi na Utoto Mtakatifu kufanyika Mwanza.

3 Ijm:  SIKUKUU YA MOYO MT. WA YESU: YUBILEI YA MAPADRE.

– Ijumaa ya Kwanza ya Mwezi – Moyo Mtakatifu wa Yesu “Benediction after Holy Mass”.

6 Jmt – 12 Jmp:  Mafungo ya Masista,  MMUU – Awamu ya I.

12 Jmp: NADHIRI ZA KWANZA NA ZA MILELE, MMUU.

18 Jms – 23 Alh: 69th PLENARY ASSEMBLY – TEC – KURASINI, DAR ES SALAAM.

19 Jmp: Uchaguzi HAWAKA  ngazi ya Parokia.

26 Jmp: ZIARA: BUSINDE PARISH: Kipaimara, Ndoa na Yubilei za Ndoa.

–  MICHANGO: St. Peter’s Pence: Kupelekwa Roma.

29 Jmo: Watakatifu Petro na Paulo.

 

JULAI 2016:  UCHAGUZI HAWAKA JIMBO.

1 Ijm: Ijumaa ya Kwanza ya Mwezi – Moyo Mtakatifu wa Yesu “Benediction after Holy Mass”.

2 Jms: Uchaguzi HAWAKA – ngazi ya Jimbo.

7 Alh: MAVUNO KIJIMBO: Kila Kigango kuwasilisha mavuno yake kwa Askofu.

– SABASABA

17 Jmp: ZIARA: KAYANGA PARISH: Kipaimara, Ndoa na Yubilei za Ndoa.

20 Jmo: ZIARA: NYAKATUNTU: Kipaimara, Ndoa na Yubilei za Ndoa.

24 Jmp: ZIARA: BUGENE  PARISH: Kipaimara, Ndoa na Yubilei za Ndoa.

31 Jmp: ZIARA: KAARO PARISH: Kipaimara, Ndoa na Yubilei za Ndoa.

AGOSTI: MWEZI WA KUTATHMINI MICHANGO YA UKUMIKA.

5 Ijm: Ijumaa ya Kwanza ya Mwezi – Moyo Mtakatifu wa Yesu “Benediction after Holy Mass”.

7 Jmp: JUMAPILI YA UPASHANAJI HABARI: Michango kuimarisha ofisi Kijimbo na Kitaifa.

ZIARA: MABIRA  PARISH: Kipaimara, Ndoa na Yubilei za Ndoa.

14 Jmp: MT. MAKSIMILIANO KOLBE: Kutangazwa kuundwa Jimbo Jipya la Kayanga (2008).

15 Jmt:  UPADRISHO: Bugomora Parish.  MIAKA 100 YA UPADRE, TANZANIA.

20 Jms: Kongamano la VIMAKA Kijimbo: Kayanga Cathedral

21 Jmp: ZIARA: NYAISHOZI  PARISH: Kipaimara, Ndoa na Yubilei za Ndoa.

28 Jmp: ZIARA: ISINGIRO PARISH: Kipaimara, Ndoa na Yubilei za Ndoa.

30 Jmn – 1 Sept. Alh: Regional Board of Seminaries (KKNS).

 

SEPTEMBA 2016: MWEZI WA KUTUKUZA MSALABA MTAKATIFU: HIJA KALVARIO-KAYUNGU.

2 Ijm: Ijumaa ya Kwanza ya Mwezi – Moyo Mtakatifu wa Yesu “Benediction after Holy Mass”.

4 Jmp: ZIARA: KIMIZA  PARISH: Kipaimara, Ndoa na Yubilei za Ndoa.

11 Jmp: ZIARA: BUGOMORA  PARISH: Kipaimara, Ndoa na Yubilei za Ndoa.

14 Jmo: KUTUKUKA MSALABA MTAKATIFU: HIJA KALVARI-KAYUNGU, Bushangaro.

15 Alh – 17 Jms: ASKOFU NA MAPADRE KUKUTANA NA MAFRATERI.

18 Jmp: ZIARA: KIRURUMA  PARISH: Kipaimara, Ndoa na Yubilei za Ndoa.

25 Jmp: ZIARA: BUGENE PARISH: Kipaimara, Ndoa na Yubilei za Ndoa.

– Yubilei ya Makatekista Maparokiani.

 

OKTOBA 2016: MWEZI WA ROZARI NA MICHANGO YA UENEZAJI INJILI TOKA KILA FAMILIA/KIGANGO.

1 Octoba: UZINDUZI WA MIAKA 100 YA UPADRE TANZANIA: RUBYA SEMINARI

2 Jmp: HIJA MUGANA

7 Ijm: Ijumaa ya Kwanza ya Mwezi – Moyo Mtakatifu wa Yesu “Benediction after Holy Mass”.

9 Jpl: ZIARA NYAKATUNTU: Kipaimara, Ndoa na Yubilei za Ndoa.

14 Ijm: Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere.

16 Jmp: ZIARA RWAMBAIZI: Kipaimara, Ndoa na Yubilei za Ndoa.

Kumbukumbu ya kifo cha Askofu Christopher Mwoleka (16.10.2002).

22 Jms: Kumbukumbu: Mt. Yohane Paulo wa Pili, Papa na Msimamizi wa Vijana.

– ZIARA: NDORAGE  PARISH: Kipaimara, Ndoa na Yubilei za Ndoa.

26 Jmo: Kutangazwa Mwenyeheri Franz Jaegerstaetter (Yegeshiteta)  (2007).

30 Jmp:ZIARA BUSHANGARO: Kipaimara, Ndoa na Yubilei za Ndoa.

NOVEMBA 2016: MWEZI WA KUZIOMBEA ROHO ZILIZOKO TOHARANI: Michango ya Nia za Misa kila siku.

1 Jmn: SHEREHE  YA WATAKATIFU WOTE.

– Kutabarukiwa Kanisa Kuu la Mt. George, Kayanga (2008).

2 Jmo: KUWAOMBEA MAREHEMU WOTE: Michango na Nia za Misa.

4 Ijm: Ijumaa ya Kwanza ya Mwezi – Moyo Mtakatifu wa Yesu “Benediction after Holy Mass”.

6 Jmp: KUZINDULIWA KWA JIMBO NA UASKOFU WA MHASHAMU ALMACHIUS RWEYONGEZA

(2008)  (Kuadhimishwa Jumapili, 13/11/2016).

11 Ijm:  BARAZA LA KICHUNGAJI.

13 Jmp: KUFUNGA MWAKA MTAKATIFU WA YUBILEI YA HURUMA YA MUNGU: KIJIMBO.

– Parokia na vigango vyake  kuwasilisha  BAHASHA YA ASKOFU/TEGEMEZA JIMBO.

20 Jmp: YESU KRISTU MFALME: Kufunga Mwaka wa Yubilei ya Huruma ya Mungu  ROMA.

22 Jmn: Mkutano wa Maaskofu na Wakubwa wa Mashirika Kanda ya Ziwa.

23 Jmo: Mkutano wa Maaskofu Kanda ya Ziwa.

24 Alh – 25 Ijm: CSSC/Zonal Policy Forum – Mwanza.

 

DESEMBA 2016:  MWEZI WA KUKAMILISHA KUNUNUA SANAMU NA HORI LA KRISMASI.

1 Alh: Siku ya kuwaombea Waathirika wa Ukimwi/VVU duniani na kumwomba

Mungu atuepushe na janga hilo hasa kwa kuzingatia Amri zake.

2 Ijm:  Ijumaa ya Kwanza ya Mwezi – Moyo Mtakatifu wa Yesu “Benediction after Holy Mass”.

6 Jmn: Kumbukumbu/Shukrani kwa Mungu: Miaka 35 ya Upadre wa Askofu Almachius

Rweyongeza.

8 Alh: BIKIRA MARIA MKINGIWA DHAMBI YA ASILI. Sherehe Nyaigando, STh  Bukoba; Rulenge, FSSB.

9 Ijm: UHURU NA JAMHURI (1961)  Kuombea Taifa letu amani na maendeleo.

11 Jmp – 17 Jms: Mafungo ya Masista MMUU, Awamu ya II.

15 Alh: TAMASHA LA 7 LA UTOTO MTAKATIFU KUFANYIKA PAROKIANI BUSINDE.

– Michango ya PMS kwa njia ya Bahasha ya kila mtoto tangia vigangoni hadi Parokiani.

 

16 Ijm: Novena ya Noeli kuanza.

24 Jms: MISA YA VIJILIA: KESHA LA NOELI:  Ubatizo wa watoto wachanga.

25 Jmp: KUZALIWA BWANA  (KRISMASI / NOELI).

26 Jmt: MISA ZA SHUKRANI NA BARAKA KWA WATOTO: MICHANGO YA PMS

KUPELEKWA ROMA.   –  Mt. Stefano Shahidi.

31 Jms: KUFUNGA MWAKA: Asubuhi Misa kama kawaida.

–  Usiku saa 2.00 – 4.00 Sala ya jioni, Rozari na Kuabudu Sakramenti Kuu.

–  Saa 4.00 – 6.15 MISA TAKATIFU: Kuaga 2016 na kukaribisha 2017.

 

 

1 JANUARI 2017 Jmp:  SHEREHE ZA MWAKA MPYA 2017: BIKIRA MARIA MAMA WA MUNGU; KUOMBA AMANI DUNIANI;  MWAKA WA 61 WA KUZALIWA ASKOFU ALMACHIUS NA SIKUKUU YA WATAKATIFU ALMACHIUS, FULGENS, ODILO NA KONKORDIUS.

 

 

MAMBO MUHIMU YA KUZINGATIA:

 1. ZIARA PAROKIANI: Askofu atafanya kazi zifuatazo:
 • Askofu atatoa Sakramenti ya Kipaimara.
 • Kila Mwanakipaimara awe na Hati ya Ubatizo, Biblia Takatifu, Rosari, Chuo Kidogo cha Sala na Nyimbo, Sala ya Mt. Mikaeli, Kitabu cha Hija, Barua ya Kichungaji, Picha ya Familia Takatifu, vitunzwe ndani ya mfuko wa plastiki ili visinyeshewe au kuchafuka.
 • Atabariki Ndoa na wenye Jubilei mbalimbali za Ndoa.
 • Ataapisha na kusimika Viongozi Wapya wa HAWAKA.
 • Atabariki wanachama wapya wa WAWATA.
 • Atatoa zawadi ya Ngao kwa Kigango Bora cha 2015 (zawadi inajumuisha 15% ya michango; sadaka na zaka; bahasha).
 • Atapitia Fomu za Taarifa za Kigango kabla ya Ziara 2016.
 • Atakagua vitabu vya Ofisi: Viwe tayari chumbani mwake.
 • Atakagua usafi wa Kanisa – mikeka, mazuria, mavazi ya Watumishi wa Misa na Vitabu vya Ibada. Atakagua STOLA ya huduma ya Sakramenti za KITUBIO na MPAKO WA WAGONJWA.
 • Atakagua HORI la Krismasi hasa sanamu zake.
 • Atakagua maendeleo ya Vituo vya Awali (Pera) watoto na walimu wao.

 

 1. BAHASHA YA TEGEMEZA JIMBO:
 • Askofu atatoa Baraka kwa washindi (2015) JNNK bora, Familia na mtu binafsi.
 • Askofu atapokea michango ya Bahasha ya Tegemeza Jimbo toka Vigango na watu binafsi.

 

 1. Michango yote ya Kijimbo, Kitaifa na Kanisa la Ulimwengu.

Stakabadhi za michango hiyo iliyotumwa kwa Mweka Hazina wa Jimbo zionyeshwe.

Jedwali linaloonyesha jinsi kila kigango kilivyochanga lionyeshwe.

 

 1. Zawadi za kumpa Askofu:
 • WAWATA – Vigango vilete zawadi ya mikeka – miekundu.
 • Kipaimara – kila mwanakipaimara nusu ndoo ya njegere au mahindi au sh. 1,000/=.
 • Wakristu wengine: Zawadi ya pesa kuanzia Tsh. 10,000/= kwa ajili ya Uinjilishaji na mawasiliano (Vocha).

 

 

 

OMNIA AD MAJOREM DEI GLORIAM

YOTE KWA SIFA NA UTUKUFU MKUU WA MUNGU

Home

You are very welcome to the online presence of Kayanga Catholic Diocese. From now on, you can find information about us online. We hope you enjoy staying with us as we will keep you up to date.

SAM_2173

Bishop Almachius Vincent Rweyongeza

map

Location of Kayanga Catholic Diocese